Native Bible

Mark 9:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini wao hawakuelewa kile alimaanisha, nao waliogopa kumuuliza maana yake.

Mark 9:32 in English

Mark 9:32 · Berean Standard Bible

But they did not understand this statement, and they were afraid to ask Him about it.

Context

30Wakaondoka huko, wakapitia Galilaya. Yesu hakutaka mtu yeyote afahamu mahali walipo, 31kwa maana alikuwa anawafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu. Nao watamuua, lakini siku tatu baada ya kuuawa atafufuka.” 32Lakini wao hawakuelewa kile alimaanisha, nao waliogopa kumuuliza maana yake. 33Basi wakafika Kapernaumu na baada ya kuingia nyumbani akawauliza, “Mlikuwa mnabishana nini kule njiani?” 34Lakini hawakumjibu, kwa sababu njiani walikuwa wakibishana kuhusu nani miongoni mwao alikuwa mkuu zaidi ya wote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.