Marko 8:36
Mark 8:36 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake?
Mark 8:36 in English
Mark 8:36 · Berean Standard Bible
What does it profit a man to gain the whole world, yet forfeit his soul?
Context
34Ndipo akauita ule umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, akasema, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. 35Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili atayaokoa. 36Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? 37Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 38Mtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.