Native Bible

Micah 1:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Usiliseme hili huko Gathi; usilie hata kidogo. Huko Beth-le-Afra gaagaa mavumbini.

Micah 1:10 in English

Micah 1:10 · Berean Standard Bible

Do not tell it in Gath;* do not weep at all. Roll in the dust in Beth-leaphrah.*

Context

8Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza; nitatembea bila viatu na tena uchi. Nitabweka kama mbweha na kuomboleza kama bundi. 9Kwa sababu jeraha lake halitibiki; limekuja Yuda. Limefika hasa kwenye lango la watu wangu, hata Yerusalemu kwenyewe. 10Usiliseme hili huko Gathi; usilie hata kidogo. Huko Beth-le-Afra gaagaa mavumbini. 11Piteni mkiwa uchi na wenye aibu, ninyi mkaao Shafiri. Wale waishio Saanani hawatatoka nje. Beth-Eseli iko katika maombolezo; kinga yake imeondolewa kwako. 12Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu wakingoja msaada, kwa sababu maangamizi yamekuja kutoka kwa Bwana, hata katika lango la Yerusalemu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.