Mathayo 7:9
Matthew 7:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Au ni nani miongoni mwenu ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe?
Matthew 7:9 in English
Matthew 7:9 · Berean Standard Bible
Which of you, if his son asks for bread, will give him a stone?
Context
7“Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. 8Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango. 9“Au ni nani miongoni mwenu ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe? 10Au mwanawe akimwomba samaki atampa nyoka? 11Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.