Mathayo 6:17
Matthew 6:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kunawa nyuso zenu
Matthew 6:17 in English
Matthew 6:17 · Berean Standard Bible
But when you fast, anoint your head and wash your face,
Context
15Lakini msipowasamehe watu wengine makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. 16“Mnapofunga, msiwe wenye huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kuwaonyesha wengine kwamba wamefunga. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha kupata thawabu yao kamilifu. 17Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kunawa nyuso zenu 18ili kufunga kwenu kusionekane na watu wengine ila Baba yenu aketiye mahali pa siri; naye Baba yenu aonaye sirini atawapa thawabu yenu kwa wazi. 19“Msijiwekee hazina duniani, mahali ambapo nondo na kutu huharibu, nao wevi huvunja na kuiba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.