Native Bible

Matthew 3:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Mto Yordani ili Yohana ambatize.

Matthew 3:13 in English

Matthew 3:13 · Berean Standard Bible

At that time Jesus came from Galilee to the Jordan to be baptized by John.

Context

11“Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu* na kwa moto. 12Pepeto lake liko mkononi mwake, naye atasafisha sakafu yake ya kupuria, na kuikusanya ngano ghalani na kuyateketeza makapi kwa moto usiozimika.” 13Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Mto Yordani ili Yohana ambatize. 14Lakini Yohana akajitahidi kumzuia, akimwambia, “Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu nikubatize?” 15Lakini Yesu akamjibu, “Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote.” Hivyo Yohana akakubali.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.