Native Bible

Matthew 23:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ninyi viongozi vipofu, mnachuja kiroboto lakini mnameza ngamia!

Matthew 23:24 in English

Matthew 23:24 · Berean Standard Bible

You blind guides! You strain out a gnat but swallow a camel.*

Context

22Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketiye juu ya kiti hicho. 23“Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnatoa zaka ya mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu zaidi ya sheria, yaani haki, huruma na uaminifu. Iliwapasa kufanya haya makuu ya sheria bila kupuuza hayo matoleo. 24Ninyi viongozi vipofu, mnachuja kiroboto lakini mnameza ngamia! 25“Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyangʼanyi na kutokuwa na kiasi. 26Ewe Farisayo kipofu! Safisha ndani ya kikombe na sahani kwanza, ndipo nje itakuwa safi pia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.