Mathayo 21:14
Matthew 21:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Vipofu na vilema wakamwendea kule Hekaluni, naye akawaponya.
Matthew 21:14 in English
Matthew 21:14 · Berean Standard Bible
The blind and the lame came to Him at the temple, and He healed them.
Context
12Yesu akaingia katika eneo la Hekalu na kuwafukuza wote waliokuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 13Akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi.” 14Vipofu na vilema wakamwendea kule Hekaluni, naye akawaponya. 15Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika. 16Wakamuuliza Yesu, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?”
Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma,
“ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao
umeamuru sifa’?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.