Mathayo 20:24
Matthew 20:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, waliwakasirikia hao ndugu wawili.
Matthew 20:24 in English
Matthew 20:24 · Berean Standard Bible
When the ten heard about this, they were indignant with the two brothers.
Context
22Yesu akawaambia, “Ninyi hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kukinywea kikombe nitakachonywea mimi?”
Wakajibu, “Tunaweza.” 23Yesu akawaambia, “Kwa kweli kikombe changu mtakinywea, lakini kuketi upande wangu wa kuume au wa kushoto si langu mimi kuwapa. Nafasi hizo ni za wale ambao wameandaliwa na Baba yangu.” 24Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, waliwakasirikia hao ndugu wawili. 25Lakini Yesu akawaita wote pamoja na kuwaambia, “Mnafahamu kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, nao wenye vyeo huonyesha mamlaka yao. 26Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.