Native Bible

Luke 9:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mtu mmoja katika ule umati wa watu akapaza sauti, akasema, “Mwalimu, naomba umwangalie mwanangu, kwani ndiye mtoto wangu wa pekee.

Luke 9:38 in English

Luke 9:38 · Berean Standard Bible

Suddenly a man in the crowd cried out, “Teacher, I beg You to look at my son, for he is my only child.

Context

36Baada ya sauti hiyo kusema, walimkuta Yesu akiwa peke yake. Wale wanafunzi wakalihifadhi jambo hili, wala kwa wakati huo hawakumwambia mtu yeyote yale waliyokuwa wameyaona. 37Kesho yake waliposhuka kutoka mlimani, alikutana na umati mkubwa wa watu. 38Mtu mmoja katika ule umati wa watu akapaza sauti, akasema, “Mwalimu, naomba umwangalie mwanangu, kwani ndiye mtoto wangu wa pekee. 39Mara kwa mara pepo mchafu humpagaa na kumfanya apige kelele, kisha humwangusha na kumtia kifafa hata akatokwa na povu kinywani. Huyo pepo mchafu anamtesa sana, na hamwachi ila mara chache. 40Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.