Native Bible

Luke 9:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yesu akawakataza wasimwambie mtu yeyote jambo hilo.

Luke 9:21 in English

Luke 9:21 · Berean Standard Bible

Jesus strictly warned them not to tell this to anyone.

Context

19Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema kwamba ni mmoja wa manabii wa kale amefufuka kutoka kwa wafu.” 20Kisha akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?” Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo* wa Mungu.” 21Yesu akawakataza wasimwambie mtu yeyote jambo hilo. 22Yesu akasema, “Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na itampasa auawe, lakini siku ya tatu kufufuliwa kutoka mauti.” 23Kisha akawaambia wote, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake kila siku, anifuate.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.