Luka 7:30
Luke 7:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Mafarisayo na wataalamu wa sheria walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokubali kubatizwa na Yohana.)
Luke 7:30 in English
Luke 7:30 · Berean Standard Bible
But the Pharisees and experts in the law rejected God’s purpose for themselves, because they had not been baptized by John.
Context
28Nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hakuna aliye mkuu kuliko Yohana. Lakini yeye aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yohana.” 29(Watu wote hata watoza ushuru waliposikia maneno ya Yesu, walikubali kwamba mpango wa Mungu ni haki, maana walikuwa wamebatizwa na Yohana. 30Lakini Mafarisayo na wataalamu wa sheria walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokubali kubatizwa na Yohana.) 31Yesu akawauliza, “Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Wanafanana na nini? 32Wao ni kama watoto waliokaa sokoni wakiitana wao kwa wao, wakisema:
“ ‘Tuliwapigia filimbi,
lakini hamkucheza;
tuliwaimbia nyimbo za maombolezo,
lakini hamkulia.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.