Luka 23:20
Luke 23:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pilato, akitaka kumwachia Yesu, akasema nao tena.
Luke 23:20 in English
Luke 23:20 · Berean Standard Bible
Wanting to release Jesus, Pilate addressed them again,
Context
18Ndipo watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “Mwondoe mtu huyo! Tufungulie Baraba!” 19(Baraba alikuwa amefungwa gerezani kwa sababu ya maasi yaliyokuwa yametokea mjini, na kwa ajili ya uuaji.) 20Pilato, akitaka kumwachia Yesu, akasema nao tena. 21Lakini wao wakaendelea kupiga kelele wakisema, “Msulubishe! Msulubishe!” 22Kwa mara ya tatu, Pilato akawauliza, “Kwani amefanya kosa gani huyu mtu? Sikuona kwake sababu yoyote inayostahili adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi, na kisha nitamwachia.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.