Luka 23:13
Luke 23:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi Pilato akawaita pamoja viongozi wa makuhani, viongozi wengine na watu,
Luke 23:13 in English
Luke 23:13 · Berean Standard Bible
Then Pilate called together the chief priests, the rulers, and the people,
Context
11Herode na askari wake wakamdhihaki Yesu na kumfanyia mzaha. Wakamvika vazi zuri sana, wakamrudisha kwa Pilato. 12Siku hiyo, Herode na Pilato wakawa marafiki; kabla ya jambo hili walikuwa na uadui kati yao. 13Basi Pilato akawaita pamoja viongozi wa makuhani, viongozi wengine na watu, 14akawaambia, “Ninyi mlimleta huyu mtu kwangu kana kwamba ni mtu anayewachochea watu ili waasi. Nimemhoji mbele yenu nami nimeona hakuna msingi wowote wa mashtaka yenu dhidi yake. 15Wala Herode hakumwona na kosa lolote, ndiyo sababu amemrudisha kwetu. Kama mnavyoona, mtu huyu hakufanya jambo lolote linalostahili kifo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.