Native Bible

Luke 22:51 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa lile sikio la yule mtu na kumponya.

Luke 22:51 in English

Luke 22:51 · Berean Standard Bible

But Jesus answered, “No more of this!” And He touched the man’s ear and healed him.

Context

49Wafuasi wa Yesu walipoona yale yaliyokuwa yanakaribia kutokea, wakasema, “Bwana, tuwakatekate kwa panga zetu?” 50Mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume. 51Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa lile sikio la yule mtu na kumponya. 52Kisha Yesu akawaambia wale viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu, pamoja na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba mimi ni mnyangʼanyi? 53Siku kwa siku nilikuwa pamoja nanyi Hekaluni lakini hamkunikamata. Lakini hii ni saa yenu, wakati giza linatawala!”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.