Luka 17:26
Luke 17:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kama ilivyokuwa siku za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Adamu.
Luke 17:26 in English
Luke 17:26 · Berean Standard Bible
Just as it was in the days of Noah, so also will it be in the days of the Son of Man:
Context
24Kwa maana kama vile umeme wa radi umulikavyo katika anga kuanzia mwisho mmoja hadi mwingine, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake. 25Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki. 26“Kama ilivyokuwa siku za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Adamu. 27Watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Noa alipoingia katika safina. Ndipo gharika ikaja na kuwaangamiza wote. 28“Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Loti: Watu walikuwa wakila na kunywa, wakinunua na kuuza, wakilima na kujenga.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.