Luka 16:7
Luke 16:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kisha akamuuliza wa pili, ‘Wewe deni lako ni kiasi gani?’ “Akajibu, ‘Vipimo 1,000* vya ngano.’ “Yule msimamizi akamwambia, ‘Chukua hati yako, andika vipimo 800!’
Luke 16:7 in English
Luke 16:7 · Berean Standard Bible
Then he asked another, ‘And how much do you owe?’ ‘A hundred measures of wheat,’* he replied. ‘Take your bill and write eighty,’ he told him.
Context
5“Kwa hiyo akawaita wadeni wote wa bwana wake, mmoja mmoja. Akamuuliza wa kwanza, ‘Deni lako kwa bwana wangu ni kiasi gani?’ 6“Akajibu, ‘Galoni 800* za mafuta ya mizeituni.’
“Msimamizi akamwambia, ‘Chukua hati ya deni lako, ibadilishe upesi, uandike galoni 400.’ 7“Kisha akamuuliza wa pili, ‘Wewe deni lako ni kiasi gani?’
“Akajibu, ‘Vipimo 1,000* vya ngano.’
“Yule msimamizi akamwambia, ‘Chukua hati yako, andika vipimo 800!’ 8“Yule bwana akamsifu yule msimamizi dhalimu kwa jinsi alivyotumia ujanja. Kwa maana watu wa dunia hii wana ujanja zaidi wanapojishughulisha na mambo ya dunia kuliko watu wa nuru. 9Nawaambia, tumieni mali ya kidunia kujipatia marafiki, ili itakapokwisha, mkaribishwe katika makao ya milele.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.