Luka 11:25
Luke 11:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye arudipo na kuikuta ile nyumba imefagiliwa na kupangwa vizuri,
Luke 11:25 in English
Luke 11:25 · Berean Standard Bible
On its return, it finds the house swept clean and put in order.
Context
23“Mtu asiyekuwa pamoja nami yu kinyume nami, na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, hutawanya. 24“Pepo mchafu amtokapo mtu, hutangatanga katika sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini hapati. Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu nilikotoka.’ 25Naye arudipo na kuikuta ile nyumba imefagiliwa na kupangwa vizuri, 26ndipo huenda na kuchukua pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza.” 27Ikawa Yesu alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katikati ya ule umati wa watu akapaza sauti akasema, “Limebarikiwa tumbo lililokuzaa na matiti uliyonyonya!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.