Native Bible

Leviticus 6:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Moto lazima uendelee kuwaka juu ya madhabahu mfululizo, kamwe usizimike.

Leviticus 6:13 in English

Leviticus 6:13 · Berean Standard Bible

The fire shall be kept burning on the altar continually; it must not be extinguished.

Context

11Kisha atayavua mavazi haya na kuvaa mengine, naye achukue yale majivu nje ya kambi na kuyapeleka mahali palipo safi kwa kawaida ya ibada. 12Moto ulio juu ya madhabahu lazima uwe unaendelea kuwaka, kamwe usizimike. Kila asubuhi kuhani ataongeza kuni na kupanga sadaka ya kuteketezwa juu ya moto, na kuteketeza mafuta ya sadaka za amani juu yake. 13Moto lazima uendelee kuwaka juu ya madhabahu mfululizo, kamwe usizimike. 14“ ‘Haya ndiyo masharti ya sadaka ya nafaka: Wana wa Aroni wataileta mbele za Bwana, mbele za madhabahu. 15Kuhani atachukua konzi ya unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote ulioko juu ya sadaka ya nafaka, ateketeze sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.