Native Bible

Leviticus 27:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu,* gera ishirini kwa shekeli.

Leviticus 27:25 in English

Leviticus 27:25 · Berean Standard Bible

Every valuation will be according to the sanctuary shekel, twenty gerahs to the shekel.*

Context

23kuhani ataamua thamani yake hadi Mwaka wa Yubile, naye huyo mtu atalazimika kulipa thamani yake siku hiyo kama kitu kitakatifu kwa Bwana. 24Katika Mwaka wa Yubile, shamba litarudishwa kwa mtu yule ambaye lilinunuliwa kutoka kwake, yule ambaye ardhi ilikuwa mali yake. 25Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu,* gera ishirini kwa shekeli. 26“ ‘Lakini hakuna mtu atakayeweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa mnyama, kwa kuwa mzaliwa wa kwanza tayari ni mali ya Bwana; awe ngʼombe au kondoo, ni wa Bwana. 27Kama ni mmoja wa wanyama walio najisi, aweza kumnunua kwa bei iliyowekwa, akiongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Kama hatamkomboa, mnyama huyo atauzwa kwa bei iliyowekwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.