Native Bible

Leviticus 26:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“ ‘Ikiwa mtafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii maagizo yangu,

Leviticus 26:3 in English

Leviticus 26:3 · Berean Standard Bible

If you follow My statutes and carefully keep My commandments,

Context

1“ ‘Msijitengenezee sanamu au kusimamisha kinyago cha kuchonga, au mnara, wala jiwe la kuabudia, na pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu na kusujudu mbele yake. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu. 2“ ‘Zishikeni Sabato zangu na kuheshimu mahali patakatifu pangu. Mimi ndimi Bwana. 3“ ‘Ikiwa mtafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii maagizo yangu, 4nitawanyeshea mvua katika majira yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake. 5Kupura nafaka kwenu kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu. Pia kuvuna zabibu kutaendelea mpaka wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.