Walawi 25:39
Leviticus 25:39 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini katikati yako, naye akajiuza kwako, usimfanye atumike kama mtumwa.
Leviticus 25:39 in English
Leviticus 25:39 · Berean Standard Bible
If a countryman among you becomes destitute and sells himself to you, then you must not force him into slave labor.
Context
37Usimkopeshe fedha ili alipe na riba, wala usimuuzie chakula kwa faida. 38Mimi ndimi Bwana Mungu wako, niliyekuleta kutoka nchi ya Misri nikupe nchi ya Kanaani, nami niwe Mungu wako. 39“ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini katikati yako, naye akajiuza kwako, usimfanye atumike kama mtumwa. 40Atatendewa kama mfanyakazi aliyeajiriwa, au kama mkazi wa muda katikati yako, naye atatumika mpaka Mwaka wa Yubile. 41Ndipo yeye na watoto wake wataachiwa, naye atarudi kwa watu wa ukoo wake, na kwenye mali ya baba zake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.