Walawi 23:34
Leviticus 23:34 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, Sikukuu ya Bwana ya vibanda itaanza, nayo itaadhimishwa kwa siku saba.
Leviticus 23:34 in English
Leviticus 23:34 · Berean Standard Bible
“Speak to the Israelites and say, ‘On the fifteenth day of the seventh month the Feast of Tabernacles * to the LORD begins, and it continues for seven days.
Context
32Ni Sabato ya mapumziko kwenu ninyi, na lazima mfunge. Tangu jioni ya siku ya tisa ya mwezi hadi jioni inayofuata, mtaishika Sabato yenu.” 33Bwana akamwambia Mose, 34“Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, Sikukuu ya Bwana ya vibanda itaanza, nayo itaadhimishwa kwa siku saba. 35Siku ya kwanza ni kusanyiko takatifu, msifanye kazi zenu za kawaida. 36Kwa siku saba toeni sadaka kwa Bwana za kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu, na mtoe sadaka kwa Bwana ya kuteketezwa kwa moto. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.