Native Bible

Leviticus 2:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ukande na kumimina mafuta juu yake; hii ni sadaka ya nafaka.

Leviticus 2:6 in English

Leviticus 2:6 · Berean Standard Bible

Crumble it and pour oil on it; it is a grain offering.

Context

4“ ‘Kama utaleta sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni, itakuwa ya unga laini: maandazi yaliyotengenezwa bila kutiwa chachu, yaliyochanganywa na mafuta, au mikate myembamba iliyotengenezwa bila kutiwa chachu, na iliyopakwa mafuta. 5Iwapo sadaka yako ya nafaka imeandaliwa kwenye kikaango, itakuwa ni ya unga laini uliochanganywa na mafuta, bila chachu. 6Ukande na kumimina mafuta juu yake; hii ni sadaka ya nafaka. 7Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa kwenye sufuria, itatengenezwa kwa unga laini na mafuta. 8Ilete hiyo sadaka ya nafaka iliyotengenezwa kwa vitu hivi kwa Bwana; mkabidhi kuhani ambaye ataipeleka madhabahuni.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.