Walawi 2:11
Leviticus 2:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“ ‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwa Bwana ni lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yoyote au asali katika sadaka itolewayo kwa Bwana kwa moto.
Leviticus 2:11 in English
Leviticus 2:11 · Berean Standard Bible
No grain offering that you present to the LORD may be made with leaven, for you are not to burn any leaven or honey as an offering made by fire to the LORD.
Context
9Naye atatoa ile sehemu ya kumbukumbu kutoka kwenye hiyo sadaka ya nafaka na kuiteketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 10Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Aroni na wanawe; ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana ya sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. 11“ ‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwa Bwana ni lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yoyote au asali katika sadaka itolewayo kwa Bwana kwa moto. 12Unaweza kuzileta kwa Bwana kama sadaka ya malimbuko, lakini haziwezi kutolewa juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kupendeza. 13Koleza sadaka zako zote za nafaka kwa chumvi. Usiache kuweka chumvi ya Agano la Mungu wako katika sadaka zako za nafaka; weka chumvi kwenye sadaka zako zote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.