Walawi 17:5
Leviticus 17:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hii ni ili Waisraeli wamletee Bwana dhabihu wanazozifanya sasa mahali pa wazi mashambani. Ni lazima wazilete kwa makuhani, yaani kwa Bwana, katika ingilio la Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu kama sadaka za amani.
Leviticus 17:5 in English
Leviticus 17:5 · Berean Standard Bible
For this reason the Israelites will bring to the LORD the sacrifices they have been offering in the open fields. They are to bring them to the priest at the entrance to the Tent of Meeting and offer them as sacrifices of peace to the LORD.
Context
3Mwisraeli yeyote atakayetoa dhabihu ya maksai, mwana-kondoo au mbuzi ndani ya kambi au nje yake, 4badala ya kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kuileta kama sadaka kwa Bwana mbele ya Maskani ya Bwana, mtu huyo atahesabiwa kuwa na hatia ya kumwaga damu; ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. 5Hii ni ili Waisraeli wamletee Bwana dhabihu wanazozifanya sasa mahali pa wazi mashambani. Ni lazima wazilete kwa makuhani, yaani kwa Bwana, katika ingilio la Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu kama sadaka za amani. 6Kuhani atanyunyiza damu kwenye madhabahu ya Bwana katika ingilio la Hema la Kukutania, na kuyateketeza mafuta ya hiyo dhabihu kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 7Hawatatoa kamwe dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi ambazo wamekuwa wakijifanyia nazo ukahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwao na kwa ajili ya vizazi vijavyo.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.