Walawi 14:50
Leviticus 14:50 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Atamchinja mmoja wa wale ndege kwenye chungu chenye maji safi.
Leviticus 14:50 in English
Leviticus 14:50 · Berean Standard Bible
and he shall slaughter one of the birds over fresh water in a clay pot.
Context
48“Lakini ikiwa kuhani atakuja kuikagua na kukuta kuwa upele haujaenea tena baada ya nyumba kupigwa lipu, ataitangaza nyumba ile kuwa safi, kwa sababu upele umekwisha. 49Ili kuitakasa nyumba hiyo, mwenye nyumba ataleta ndege wawili, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo. 50Atamchinja mmoja wa wale ndege kwenye chungu chenye maji safi. 51Kisha atachukua mti wa mwerezi, hisopo, kitani nyekundu na ndege aliye hai, na kuvitumbukiza ndani ya damu ya ndege aliyechinjwa pamoja na maji safi, na kuinyunyizia nyumba ile mara saba. 52Ataitakasa nyumba kwa damu ya yule ndege, maji safi, ndege aliye hai, mti wa mwerezi, hisopo na kitani nyekundu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.