Walawi 13:50
Leviticus 13:50 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kuhani atachunguza upele huo na kukitenga kifaa hicho kwa siku saba.
Leviticus 13:50 in English
Leviticus 13:50 · Berean Standard Bible
And the priest is to examine the mildew and isolate the contaminated fabric for seven days.
Context
48lolote lililofumwa au kusokotwa likiwa la kitani au la sufu, ngozi yoyote au chochote kilichotengenezwa kwa ngozi, 49tena kama maambukizo kwenye vazi, au ngozi, au lililofumwa au kusokotwa, au kifaa chochote cha ngozi, ni rangi ya kijani au nyekundu, huo ni upele unaoenea na ni lazima kuhani aonyeshwe. 50Kuhani atachunguza upele huo na kukitenga kifaa hicho kwa siku saba. 51Siku ya saba atakichunguza, na kama upele umeenea kwenye nguo, au kifaa kilichofumwa au kusokotwa, au ngozi, kwa vyovyote vile itumikavyo, ni upele uangamizao, kifaa hicho ni najisi. 52Ni lazima aichome hiyo nguo, ikiwa ni ya sufu ama kitani iliyofumwa ama kusokotwa, ama chombo chochote cha ngozi chenye maambukizo, kwa kuwa ni upele unaoangamiza; chombo chote ni lazima kichomwe moto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.