Walawi 13:35
Leviticus 13:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini ikiwa upele utaenea juu ya ngozi baada ya kutangazwa kuwa safi,
Leviticus 13:35 in English
Leviticus 13:35 · Berean Standard Bible
If, however, the scaly outbreak spreads further on the skin after his cleansing,
Context
33mtu huyo ni lazima anyolewe, isipokuwa mahali palipo na ugonjwa, naye kuhani atamtenga kwa siku nyingine saba. 34Siku ya saba kuhani atachunguza tena ule upele; ikiwa haujaenea kwenye ngozi na hakuna shimo mahali pale, kuhani atamtangaza kuwa safi. Lazima afue nguo zake, naye atakuwa safi. 35Lakini ikiwa upele utaenea juu ya ngozi baada ya kutangazwa kuwa safi, 36kuhani atamchunguza, na kama upele umeenea kwenye ngozi, kuhani hana haja ya kutazama kama kuna nywele za manjano, mtu huyo ni najisi. 37Hata hivyo, katika uchunguzi wake akiona hapajabadilika, na nywele nyeusi zimeota juu yake, upele umepona. Yeye si najisi, kuhani atamtangaza kuwa safi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.