Walawi 11:30
Leviticus 11:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
guruguru, kenge, mijusi ya ukutani, goromoe na kinyonga.
Leviticus 11:30 in English
Leviticus 11:30 · Berean Standard Bible
the gecko, the monitor lizard, the common lizard, the skink, and the chameleon.
Context
28Yeyote atakayebeba mizoga yao ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Wanyama hawa ni najisi kwenu. 29“ ‘Kuhusu wanyama watambaao juu ya ardhi, hawa ni najisi kwenu: kicheche, panya, aina yoyote ya mijusi mikubwa, 30guruguru, kenge, mijusi ya ukutani, goromoe na kinyonga. 31Hao wote watambaao juu ya ardhi ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni. 32Ikiwa mmoja wao atakufa na kuangukia juu ya kitu fulani, chombo hicho, hata kikiwa cha matumizi gani, kitakuwa najisi, kiwe kimetengenezwa kwa mti, nguo, ngozi au gunia. Kiweke ndani ya maji; kitakuwa najisi mpaka jioni, kisha kitakuwa safi tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.