Yoshua 9:2
Joshua 9:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
wakajiunga pamoja ili kupigana vita dhidi ya Yoshua na Israeli.
Joshua 9:2 in English
Joshua 9:2 · Berean Standard Bible
they came together to wage war against Joshua and Israel.
Context
1Basi ikawa wafalme wote waliokuwa magharibi mwa Yordani waliposikia juu ya haya yote, wale waliokuwa katika nchi ya vilima, upande wa magharibi mwa vilima na katika pwani yote ya hiyo Bahari Kuu,* hadi kufikia Lebanoni (wafalme wa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi), 2wakajiunga pamoja ili kupigana vita dhidi ya Yoshua na Israeli. 3Hata hivyo, watu wa Gibeoni waliposikia juu ya hayo yote Yoshua aliyowatendea watu wa Yeriko na Ai, 4nao wakaamua kufanya hila: Wakajifanya kama wajumbe wakiwa na punda waliobebeshwa mizigo wakiwa na magunia yaliyochakaa na viriba vya mvinyo vikuukuu vyenye nyufa zilizozibwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.