Yoshua 8:23
Joshua 8:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini wakamchukua mfalme wa Ai akiwa hai na kumleta kwa Yoshua.
Joshua 8:23 in English
Joshua 8:23 · Berean Standard Bible
But they took the king of Ai alive and brought him to Joshua.
Context
21Basi Yoshua na Israeli wote walipoona kwamba waviziaji wameshauteka mji na moshi ulikuwa unapaa juu kutoka kwenye mji, wakawageukia watu wa Ai na kuwashambulia. 22Wale waviziaji nao pia wakatoka nje ya mji dhidi yao, hivi kwamba wakashikiwa katikati, Waisraeli wakiwa pande zote mbili. Israeli wakawaua, bila kuwaachia yeyote aliyenusurika wala aliyetoroka. 23Lakini wakamchukua mfalme wa Ai akiwa hai na kumleta kwa Yoshua. 24Israeli ilipomaliza kuwaua wanaume wote wa Ai katika mashamba na jangwani walipokuwa wamewafukuzia, na baada ya kila mmoja wao kuuawa kwa upanga, Waisraeli wote wakarudi Ai na kuwaua wale waliokuwa wamebakia mjini. 25Watu kumi na mbili elfu, waume kwa wake, waliangamia siku ile, yaani watu wote wa Ai.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.