Yoshua 7:10
Joshua 7:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana akamwambia Yoshua, “Simama! Unafanya nini hapo chini kifudifudi?
Joshua 7:10 in English
Joshua 7:10 · Berean Standard Bible
But the LORD said to Joshua, “Stand up! Why have you fallen on your face?
Context
8Ee Bwana, niseme nini sasa, ikiwa sasa Israeli ameshafukuzwa na adui zake? 9Wakanaani na watu wengine wa nchi watasikia habari hii, nao watatuzunguka na kutufutilia jina letu duniani. Utafanya nini basi kwa ajili ya jina lako mwenyewe lililo kuu?” 10Bwana akamwambia Yoshua, “Simama! Unafanya nini hapo chini kifudifudi? 11Israeli ametenda dhambi. Wamekiuka agano langu nililowaamuru kulishika. Wamechukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu, wameiba, wamesema uongo, wameviweka pamoja na mali zao. 12Ndiyo sababu Waisraeli hawawezi kusimama dhidi ya adui zao. Wanawapa visogo na kukimbia kwa kuwa wanastahili maangamizi. Sitakuwa pamoja nanyi tena mpaka mwangamize kila kitu miongoni mwenu kilichotengwa kwa maangamizi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.