Native Bible

Joshua 23:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo kuweni waangalifu sana kumpenda Bwana Mungu wenu.

Joshua 23:11 in English

Joshua 23:11 · Berean Standard Bible

Therefore watch yourselves carefully, that you love the LORD your God.

Context

9“Bwana amewafukuza mbele yenu mataifa makubwa na yenye nguvu, mpaka siku ya leo hakuna yeyote aliyeweza kusimama mbele yenu. 10Mtu mmoja miongoni mwenu anafukuza watu elfu, kwa kuwa Bwana Mungu wenu anawapigania, kama alivyoahidi. 11Kwa hiyo kuweni waangalifu sana kumpenda Bwana Mungu wenu. 12“Lakini ikiwa mtageuka na kushikamana na mabaki ya mataifa haya yaliyosalia katikati yenu na kama mtaoana na kushirikiana nao, 13basi mwe na hakika kuwa Bwana Mungu wenu hatawafukuza tena mataifa hayo mbele yenu. Badala yake, watakuwa tanzi na mitego kwenu, mijeledi migongoni mwenu, na miiba machoni mwenu, mpaka mwangamie kutoka nchi hii nzuri, ambayo Bwana Mungu wenu amewapa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.