Yoshua 21:9
Joshua 21:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kutoka makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina
Joshua 21:9 in English
Joshua 21:9 · Berean Standard Bible
From the tribes of Judah and Simeon, they designated these cities by name
Context
7Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni. 8Kwa hiyo Waisraeli wakawapa Walawi miji hii pamoja na sehemu zake za malisho, kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru kupitia kwa Mose. 9Kutoka makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina 10(miji hii walipewa wazao wa Aroni ambao walitokana na koo za Wakohathi wa Walawi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia): 11Waliwapa Kiriath-Arba (yaani Hebroni), pamoja na sehemu zake za malisho zilizoizunguka, katika nchi ya vilima ya Yuda. (Arba alikuwa baba wa Anaki.)
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.