Yoshua 18:2
Joshua 18:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
lakini palikuwa bado makabila saba ya Israeli ambayo yalikuwa hayajapokea urithi wao.
Joshua 18:2 in English
Joshua 18:2 · Berean Standard Bible
there were still seven tribes of Israel who had not yet received their inheritance.
Context
1Kusanyiko lote la Waisraeli likakusanyika huko Shilo na kusimamisha Hema la Kukutania. Nchi ikawa chini ya utawala wao, 2lakini palikuwa bado makabila saba ya Israeli ambayo yalikuwa hayajapokea urithi wao. 3Hivyo Yoshua akawaambia Waisraeli, “Je, mtasubiri hata lini ili kuingia kumiliki nchi ambayo Bwana, Mungu wa baba zenu, amewapa? 4Chagueni watu watatu kutoka kwenye kila kabila. Nitawatuma hao watu kukagua hiyo nchi na kuniandikia mapendekezo ya mgawanyo wa urithi wa kila kabila. Nao watanirudia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.