Yoeli 1:9
Joel 1:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji zimekatiliwa mbali kutoka nyumba ya Bwana. Makuhani wanaomboleza, wale wanaohudumu mbele za Bwana.
Joel 1:9 in English
Joel 1:9 · Berean Standard Bible
Grain and drink offerings have been cut off from the house of the LORD; the priests are in mourning, those who minister before the LORD.
Context
7Limeharibu mizabibu yangu
na kuangamiza mitini yangu.
Limebambua magome yake
na kuyatupilia mbali,
likayaacha matawi yake yakiwa meupe. 8Omboleza kama bikira aliyevaa nguo ya gunia
anayehuzunika kwa ajili ya mume wa ujana wake. 9Sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji
zimekatiliwa mbali kutoka nyumba ya Bwana.
Makuhani wanaomboleza,
wale wanaohudumu mbele za Bwana. 10Mashamba yameharibiwa,
ardhi imekauka;
nafaka imeharibiwa,
mvinyo mpya umekauka,
mafuta yamekoma. 11Kateni tamaa, enyi wakulima,
lieni, enyi mlimao mizabibu;
huzunikeni kwa ajili ya ngano na shayiri,
kwa sababu mavuno ya shambani yameharibiwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.