Native Bible

Job 1:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Siku moja wana wa Mungu* walikwenda kujionyesha mbele za Bwana. Shetani* naye akaja pamoja nao.

Job 1:6 in English

Job 1:6 · Berean Standard Bible

One day the sons of God came to present themselves before the LORD, and Satan * also came with them.

Context

4Wanawe walikuwa na desturi ya kufanya karamu katika nyumba zao kwa zamu, nao wangewaalika umbu zao watatu ili kula na kunywa pamoja nao. 5Wakati kipindi cha karamu kilimalizika, Ayubu angetuma waitwe na kuwafanyia utakaso. Angetoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya kila mmoja wao asubuhi na mapema, akifikiri, “Pengine wanangu wametenda dhambi na kumlaani Mungu mioyoni mwao.” Hii ilikuwa ndiyo desturi ya kawaida ya Ayubu. 6Siku moja wana wa Mungu* walikwenda kujionyesha mbele za Bwana. Shetani* naye akaja pamoja nao. 7Bwana akamwambia Shetani, “Umetoka wapi?” Shetani akamjibu Bwana, “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.” 8Ndipo Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuepukana na uovu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.