Yohana 5:3
John 5:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani, vipofu, viwete, na waliopooza [wakingojea maji yatibuliwe.
John 5:3 in English
John 5:3 · Berean Standard Bible
On these walkways * lay a great number of the sick, the blind, the lame, and the paralyzed.*
Context
1Baada ya haya, kulikuwa na Sikukuu ya Wayahudi, naye Yesu akapanda kwenda Yerusalemu. 2Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, palikuwa na bwawa moja lililoitwa kwa Kiebrania Bethzatha,* ambalo lilikuwa limezungukwa na kumbi tano. 3Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani, vipofu, viwete, na waliopooza [wakingojea maji yatibuliwe. 4Kwa maana malaika alikuwa akishuka wakati fulani, akayatibua maji. Yule aliyekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao]. 5Mtu mmoja alikuwako huko ambaye alikuwa ameugua kwa miaka thelathini na minane.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.