Yohana 3:28
John 3:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema, ‘Mimi si Kristo,* ila nimetumwa nimtangulie.’
John 3:28 in English
John 3:28 · Berean Standard Bible
You yourselves can testify that I said, ‘I am not the Christ, but am sent ahead of Him.’
Context
26Wakamwendea Yohana wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ngʼambo ya Mto Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!” 27Yohana akawajibu, “Hakuna mtu yeyote awezaye kupata kitu chochote isipokuwa kile tu alichopewa kutoka mbinguni. 28Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema, ‘Mimi si Kristo,* ila nimetumwa nimtangulie.’ 29Bibi arusi ni wa bwana arusi. Lakini rafiki yake bwana arusi anayesimama karibu naye na kusikiliza kutoka kwake, hufurahi sana aisikiapo sauti ya bwana arusi. Kwa sababu hii furaha yangu imekamilika. 30Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kuwa mdogo.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.