Yohana 21:5
John 21:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akawaambia, “Wanangu, je, mna samaki wowote?” Wakamjibu, “La.”
John 21:5 in English
John 21:5 · Berean Standard Bible
So He called out to them, “Children, do you have any fish?” “No,” they answered.
Context
3Simoni Petro akawaambia wenzake, “Mimi naenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua, lakini usiku ule hawakupata chochote. 4Mara baada ya kupambazuka, Yesu akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Yesu. 5Yesu akawaambia, “Wanangu, je, mna samaki wowote?”
Wakamjibu, “La.” 6Akawaambia, “Shusheni nyavu upande wa kuume wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Wakashusha nyavu na tazama wakapata samaki wengi mno hata wakashindwa kuvutia zile nyavu zilizojaa samaki ndani ya mashua. 7Yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro, “Huyu ni Bwana!” Simoni Petro aliposikia haya, akajifunga nguo yake kwa kuwa alikuwa uchi, naye akajitosa baharini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.