Yohana 18:4
John 18:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akijua yale yote yatakayompata, akajitokeza mbele yao akawauliza, “Mnamtafuta nani?”
John 18:4 in English
John 18:4 · Berean Standard Bible
Jesus, knowing all that was coming upon Him, stepped forward and asked them, “Whom are you seeking?”
Context
2Basi Yuda, yule aliyemsaliti alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana humo na wanafunzi wake mara kwa mara. 3Hivyo Yuda akaja bustanini. Aliongoza kikosi cha askari wa Kirumi, na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Nao walikuwa wamechukua taa, mienge na silaha. 4Yesu akijua yale yote yatakayompata, akajitokeza mbele yao akawauliza, “Mnamtafuta nani?” 5Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.”
Yesu akawajibu, “Mimi ndiye.” Yuda, yule aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. 6Yesu alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.