Yohana 13:23
John 13:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mmoja wa wanafunzi wake ambaye Yesu alimpenda sana, alikuwa ameegama kifuani mwa Yesu.
John 13:23 in English
John 13:23 · Berean Standard Bible
One of His disciples, the one whom Jesus loved, was reclining at His side.*
Context
21Baada ya kusema haya, Yesu alifadhaika sana moyoni, akasema, “Amin, amin nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.” 22Wanafunzi wake wakatazamana bila kujua kuwa alikuwa anamsema nani. 23Mmoja wa wanafunzi wake ambaye Yesu alimpenda sana, alikuwa ameegama kifuani mwa Yesu. 24Simoni Petro akampungia mkono yule mwanafunzi, akamwambia, “Muulize anamaanisha nani.” 25Yule mwanafunzi akamwegemea Yesu, akamuuliza, “Bwana, tuambie, ni nani?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.