Yohana 11:53
John 11:53 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo tangu siku hiyo wakawa wanafanya mipango ili wamuue Yesu.
John 11:53 in English
John 11:53 · Berean Standard Bible
So from that day on they plotted to kill Him.
Context
51Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama kuhani mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Yesu angelikufa kwa ajili ya taifa la Wayahudi, 52wala si kwa ajili ya taifa hilo pekee, bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja. 53Hivyo tangu siku hiyo wakawa wanafanya mipango ili wamuue Yesu. 54Kwa hiyo Yesu akawa hatembei hadharani miongoni mwa Wayahudi, bali alijitenga akaenda sehemu iliyo karibu na jangwa kwenye kijiji kiitwacho Efraimu. Akakaa huko na wanafunzi wake. 55Basi Pasaka ya Wayahudi ilipokuwa imekaribia, watu wengi walitoka vijijini wakaenda Yerusalemu kabla ya Pasaka ili wakajitakase.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.