Yohana 11:48
John 11:48 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama tukimwacha aendelee hivi, kila mtu atamwamini, nao Warumi watakuja na kupaharibu mahali petu patakatifu na taifa letu.”
John 11:48 in English
John 11:48 · Berean Standard Bible
If we let Him go on like this, everyone will believe in Him, and then the Romans will come and take away both our place and our nation.”
Context
46Lakini baadhi yao wakaenda kwa Mafarisayo na kuwaambia mambo Yesu aliyoyafanya. 47Kwa hiyo viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakaita mkutano wa baraza.
Wakaulizana, “Tufanyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi. 48Kama tukimwacha aendelee hivi, kila mtu atamwamini, nao Warumi watakuja na kupaharibu mahali petu patakatifu na taifa letu.” 49Mmoja wao aliyeitwa Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu mwaka huo, akasema, “Ninyi hamjui kitu chochote! 50Hamjui kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa lote liangamie?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.