Yeremia 7:27
Jeremiah 7:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Utakapowaambia haya yote, hawatakusikiliza; utakapowaita, hawatajibu.
Jeremiah 7:27 in English
Jeremiah 7:27 · Berean Standard Bible
When you tell them all these things, they will not listen to you. When you call to them, they will not answer.
Context
25Tangu wakati ule baba zenu walipotoka Misri hadi sasa, siku baada ya siku, tena na tena nimewatumia watumishi wangu manabii. 26Lakini hawakunisikiliza wala hawakujali. Walikuwa na shingo ngumu na kufanya maovu kuliko baba zao.’ 27“Utakapowaambia haya yote, hawatakusikiliza; utakapowaita, hawatajibu. 28Kwa hiyo waambie, ‘Hili ni taifa ambalo halimtii Bwana, Mungu wao, wala kukubali maonyo. Kweli imekufa, imetoweka midomoni mwao. 29Nyoeni nywele zenu na kuzitupa, ombolezeni katika miinuko iliyo kame, kwa kuwa Bwana amekikataa na kukiacha kizazi hiki kilichomkasirisha.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.