Native Bible

Jeremiah 37:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada ya jeshi la Wakaldayo kujiondoa kutoka Yerusalemu kwa sababu ya jeshi la Farao,

Jeremiah 37:11 in English

Jeremiah 37:11 · Berean Standard Bible

When the Chaldean army withdrew from Jerusalem for fear of Pharaoh’s army,

Context

9“Hili ndilo Bwana asemalo: Msijidanganye wenyewe mkifikiri, ‘Hakika Wakaldayo watatuacha na kwenda zao.’ Hakika hawatawaacha! 10Hata kama mngelishinda jeshi lote la Wakaldayo linalowashambulia ninyi, na wakawa ni watu waliojeruhiwa tu waliobaki kwenye mahema yao, wangetoka na kuuchoma mji huu moto.” 11Baada ya jeshi la Wakaldayo kujiondoa kutoka Yerusalemu kwa sababu ya jeshi la Farao, 12Yeremia akaanza kuondoka mjini ili kwenda nchi ya Benyamini ili akapate sehemu yake ya milki miongoni mwa watu huko. 13Lakini alipofika kwenye Lango la Benyamini, mkuu wa walinzi, ambaye jina lake lilikuwa Iriya mwana wa Shelemia mwana wa Hanania, akamkamata Yeremia na kusema, “Wewe unakwenda kujiunga na Wakaldayo!”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.