Yeremia 31:25
Jeremiah 31:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitawaburudisha waliochoka na kuwatuliza walio na huzuni.”
Jeremiah 31:25 in English
Jeremiah 31:25 · Berean Standard Bible
for I will refresh the weary soul and replenish all who are weak.”
Context
23Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo, “Nitakapowarudisha toka nchi ya kutekwa kwenu, watu walio katika nchi ya Yuda na miji yake kwa mara nyingine tena watatumia maneno haya: ‘Bwana akubariki, ee makao ya haki, ee mlima mtakatifu.’ 24Watu wataishi pamoja katika Yuda na miji yake yote, wakulima na wote wanaohamahama na mifugo yao. 25Nitawaburudisha waliochoka na kuwatuliza walio na huzuni.” 26Kwa jambo hili niliamka na kuangalia pande zote. Usingizi wangu ulikuwa mtamu kwangu. 27Bwana asema, “Siku zinakuja, nitakapoongeza idadi ya watu, na kuzidisha hesabu ya mifugo katika nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.