Yeremia 28:10
Jeremiah 28:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha nabii Hanania akaiondoa nira iliyokuwa shingoni mwa Yeremia na kuivunja,
Jeremiah 28:10 in English
Jeremiah 28:10 · Berean Standard Bible
Then the prophet Hananiah took the yoke off the neck of Jeremiah the prophet and broke it.
Context
8Tangu mwanzo, manabii waliokutangulia wewe na mimi walitabiri vita, maafa na tauni dhidi ya nchi nyingi na falme kubwa. 9Lakini nabii atakayetabiri amani atatambuliwa kuwa kweli ametumwa na Bwana ikiwa unabii wake utatimia.” 10Kisha nabii Hanania akaiondoa nira iliyokuwa shingoni mwa Yeremia na kuivunja, 11naye akasema mbele ya watu wote, “Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Vivi hivi ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo za mataifa katika muda huu wa miaka miwili.’ ” Alipofanya hivi, nabii Yeremia akaondoka zake. 12Kitambo kidogo baada ya nabii Hanania kuivunja nira kutoka shingo ya nabii Yeremia, neno la Bwana likamjia Yeremia:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.