Yeremia 27:17
Jeremiah 27:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Msiwasikilize. Mtumikieni mfalme wa Babeli, nanyi mtaishi. Kwa nini mji huu uwe magofu?
Jeremiah 27:17 in English
Jeremiah 27:17 · Berean Standard Bible
Do not listen to them. Serve the king of Babylon and live! Why should this city become a ruin?
Context
15‘Sikuwatuma hao,’ asema Bwana. ‘Wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo, nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia, ninyi pamoja na manabii wanaowatabiria.’ ” 16Kisha nikawaambia makuhani na watu hawa wote, “Hili ndilo asemalo Bwana: Msiwasikilize manabii wanaosema, ‘Hivi karibuni sana vyombo vya nyumba ya Bwana vitarudishwa kutoka Babeli.’ Wanawatabiria ninyi uongo. 17Msiwasikilize. Mtumikieni mfalme wa Babeli, nanyi mtaishi. Kwa nini mji huu uwe magofu? 18Kama wao ni manabii na wanalo neno la Bwana, basi na wamsihi Bwana Mwenye Nguvu Zote ili vyombo vilivyobaki katika nyumba ya Bwana na katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na katika Yerusalemu visipelekwe Babeli. 19Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote kuhusu zile nguzo, ile Bahari, vile vishikizo viwezavyo kuhamishika, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.